IQNA

Qurani Tukufu

Qari wa Qur’ani wa Iran apokelewa kwa ukarimu nchini Serbia

21:56 - April 17, 2023
Habari ID: 3476882
TEHRAN (IQNA) - Waislamu nchini Serbia walipokea kwa furaha qari na mhifadhi wa Qur’an kutoka Iran Mahmoud Noruzi Farahani nchini humo.

Noruzi Farahani alitumwa katika nchi hiyo ya Ulaya na Jumuiya ya Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu kwa ajili ya usomaji wa Qur'ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alihudhuria programu mbalimbali za Qur'ani zilizoandaliwa katika miji kadhaa na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Serbia.

Misikiti katika mji mkuu Belgrade pamoja na Nis, Leskovac, na Bor iliandaa hafla za Qur’ani Tukufu.

Katika mpango huo mjini Bor, Balozi wa Iran nchini Serbia Rashid Hassanpour na Mwambata wa Utamaduni wa Iran Amir Pourpezeshk pia walihudhuria kwa mwaliko wa kiongozi wa sala ya Ijumaa wa jiji hilo.

Akihutubia katika hafla hiyo, Hassanpour alifafanua kuhusu sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuimarisha umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Pia alisisitiza dhamira ya nchi ya kuendeleza maingiliano na uhusiano, hasa katika nyanja za kitamaduni, na Waislamu wote duniani.

Mufti wa Belgrade Mustafa Jusufspahic, ambaye pia alikuwepo katika mpango huo, katika hotuba yake alishukuru uwepo wa wajumbe na qari wa Iran katika hafla hiyo ya Qur'ani.

Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Iran hutuma qaris katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kusoma Qur'ani Tukufu.

4134828

captcha