IQNA

Historia ya Uislamu

Jumba la Makumbusho la Louvre laonyesha kurasa za Msahafu wa kale

11:26 - January 02, 2023
Habari ID: 3476344
TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho La Louvre la Paris limefungua maonyesho mapya ambayo kwa kiasi fulani yanaonyesha baadhi ya kurasa za mojawapo ya nakala kongwe zaidi za Qur’ani Tukufu.

Maonyesho hayo yaliyopewa jina la ‘Uzuri Katika Chemichemi za Jangwa la  Uzbekistan’ yanajumuisha zaidi ya kazi 170 za historia ya nchi hiyo zikiwemo sanaa zinazosifika za ukutani, sanamu za Kibudha, na vitu vilivyokuwa vikitumiwa kila siku katika ustaarabu wa kale.

Kurasa mbili za Msahafu wa wa Katta Langar mojawapo ya hati za mwanzo kabisa za Qur'ani Tukufu zilizosalia duniani zikirejea siku za mwanzo za Uislamu ni kati ya vivutio vikuu katika maonyesho hayo. Kwa karne nyingi iliwekwa salama juu ya mlima. Msahafu huo umeandikwa kwenye ngozi katika aina moja ya zamani zaidi ya maandishi ya Kiarabu-Kufi na Hijazi kwenye ukurasa wa wastani wa inchi 21 kwa 14). Kwa muda mrefu, nakala hii ya Qur'ani Tukufu ilihifadhiwa katika msikiti wa Langar Ota wa Uzbekistan katika wilaya ya Qamashi ya mkoa wa Kashkadarya.

Mwanaakiolojia Rocco Rante, ambaye amekuwa akifanya kazi na kuchimba katika Chemichemi ya Jangwani ya Bukhara ya Uzbekistan tangu 2009 ndiye msimamizi mwenza wa maonyesho hayo. Uzbekistan ilikuwa kivutio kikuu katika njia ya biashara ya Barabara ya Hariri inayounganisha Mediterania na Mashariki ya Mbali.

Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano na Jumba la Makumbusho la Louvre na Wakfu wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni wa Uzbekistan. Maonyesho hayo yanakaribisha wageni katika safari ya kisiasa na kihistoria ya miaka 1600 kupitia ustaarabu wa Uzbekistan, kuanzia karne ya kwanza KK.

Maonyesho hayo yataonyeshwa kwenye Jumba la Makumbusho la Louvre mjini Paris hadi tarehe 6 Machi 2023. Maonyesho mengine yanayoendelea yenye anuani ya, "Barabara ya Samarkand: Miujiza ya Hariri na Dhahabu,” pia yanaonyesha urithi wa kitamaduni wa Uzbekistan. Maonyesho katika Jumba la Makumbusho la Louvre yanaangazia historia ya Uzbekistan kutoka karne ya tano na sita KK hadi enzi ya Watimuridi, na pia Taasisi ya Ulimwengu wa Kiarabu in maonyesho kutoka karne ya 19 hadi katikati ya 20, na vile vile picha za kuchora za Turkestan Avant-Garde kutoka kwa mkusanyiko wa makumbusho ya serikali ya Uzbekistan.

3481891

captcha