IQNA

Harakati ya Kiislamu Nigeria

Sheikh Zakzaky asimulia tukio la mauaji ya Zaria nchini Nigeria katika kumbukizi ya waka wa saba

18:49 - December 13, 2022
Habari ID: 3476244
TEHRAN (IQNA) – Katika kumbukumbu ya miaka 7 ya mauaji ya umati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Nigeria huko Zaria, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) alisimulia matukio ya siku hizo katika mahojiano.

Mwezi Disemba 2015, Jeshi la Nigeria lilivamia makazi ya Shaykh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu katika mji wa Zaria nchini Nigeria. Wanajeshi hao waliuawa mamia ya Waislamu na kumjeruhi vibaya Sheikh Zakzaky na mke wake.

Hizi ni baadhi ya dondoo za mahojiano hayo:

"Hiki ni kisa kirefu sana. Labda naweza kusema haikuwa Jumamosi ambapo tukio lilianza. Lilianza kabla ya wakati huo. Maandamano ya Arba'in yalifanyika siku tisa kabla ya shambulio. Na tulipoanza safari ya Arbain, tulipata taarifa kuwa walikusudia kutushambulia,” alisema.

"Na waliapa kwamba hawataruhusu washiriki wa matembezi ya Arbain kuingia Zaria, na hata wasafiri wakiingia watawamaliza mara moja na kwa wote, na ikiwa baadhi yao walifanikiwa kutoka Zaria, watahakikisha kwamba wanawashambulia wakirudi na kuwamaliza. Walifanya mpango. Na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, tulifaulu kuendesha Arbain,” aliongeza.

Kwingineko, Shughuli ya kuwakumbuka mashahidi waliouawa na jeshi la Nigeria miaka saba iliyopita katika mji wa Zaria imefanyika katika Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Ridha (AS) katika mji mtakatifu wa Mashhad ulioko kaskazini mwa Iran.

Hujjatul Islam Sayyid Mohammad Zulqari, Mkurugenzi wa Masuala ya Mazuwari (wafanyaziara) wasio Wairani katika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS), amesema katika shughuli hiyo kwamba, Uislamu ulipelekwa Afrika na wahajiri walioelekea Uhabeshi kabla ya kuingia Madina kama mji mkuu wa serikali ya Kiislamu wakati wa enzi ya Mtume (SAW); kwa sababu hiyo wanazuoni wa Kiafrika wanalitambua bara hilo kuwa makazi na nyumba ya kwanza ya Uislamu.

Sayyid Mohammad Zulqari amesema kuwa mapenzi ya Waafrika kwa Ahlubaiti wa Mtume (SAW) yamekita mizizi ndani ya nyoyo za Waislamu wa Afrika kiasi kwamba yameziathiri tamaduni zao za kwa maadili na mafunzo Ahlul-Bait (AS), na jambo hilo limekuwa na taathira katika kustawisha utamaduni wa Ahlul-Bait (AS) na kupambana na dhulma.

3481654

captcha