Katika chapisho kupitia Facebook mnamo Jumatatu (Aprili 18) usiku, Ismail Sabri Yaakob alisema mwezi mtukufu wa Ramadhani ni moja ya nyakati bora kwa Waislamu kuelewa yaliyomo katika Kitabu Kitakatifu ili waweze kuishi maisha bora ya mja wa Mwenyezi Mungu.
Amesema Mtume Muhammad SAW aliteremshiwa Qur'ani Tukufu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Aidha amesema 'Alhamdulillah, kipindi cha janga la corona kimetupatia fursa ya kusoma zaidi aya za Qur'ani Tukufu'.
Chapisho hilo la Facebook pia liliambatanishwa na bango la salamu za Nuzul Al-Quran kutoka kwa waziri mkuu.
Nuzul al-Quran inahusu tukio ambapo aya ya kwanza ya Quran iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika pango la Hira.
3478553