IQNA

Saudi Arabia yaondoa marufuku ya matangazo ya moja kwa moja ya Sala baada ya kukosolewa

12:00 - March 25, 2022
Habari ID: 3475074
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia ilithibitisha kwamba matangazo ya moja kwa moja ya au mubashara ya Misikiti Miwili Mitakatifu huko Makka na Madina yataendelea wakati wa mwezi wa Ramadhani baada ya marufuku iliyotangazwa awali kuzua ukosoaji.

Siku ya Jumatano, Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Mwongozo ilitangaza kwamba misikiti nchini Saudi Arabia haitaruhusiwa kurusha mubashara Sala kwenye vituo vya habari wakati wa Mwezi Mtukufu Ramadhani mwaka huu.

Taarifa hiyo ilikuwa sehemu ya taarifa pana ya kutoa ushauri kwa wasimamizi wa misikiti wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Iliwataka wasimamizi wa misikiti kutotumia kamera misikitini wakati imamu akiwaongoza waumini katika na pia kutosambaza  picha za sala kwenye vyomb vyovyote  vya habari ".

Pia iliwahimiza waumini kuepuka kuleta watoto ambao wanaweza kuwa wasumbufu, na kuwashauri wale wanaopanga kuandaa futari kwa waumini kwamba walihitaji kutuma maombi ili wapate idhini

Ingawa miongozo mingi haikupingwa lakini mwongozo kuhusu marufuku ya upigaji picha na kutangaza mubasara sala misikitini ni uamuzi ambao umeibua mgawanyika na hisia mseto huku wengi wakikosoa muongozo huo.

Wakati wa Ramadhani, ni jambo la kawaida kwa Waislamu ulimwenguni kote kutazama video za moja kwa moja kutoka Msikiti Mkuu wa Makkah, huku waumini wakitembea kuzunguka Kaaba -Tawaf - na kushiriki katika sala za kila siku kwenye Msikiti Mtakatifu zaidi wa Uislamu.

Pia ni jambo la kawaida katika mwezi mtukufu kutazama matangazo ya moja kwa moja kutoka Al-Masjid an-Nabawi (Msikiti wa Mtume), eneo la pili kwa utakatifu katika Uislamu, katika mji wa Madina, magharibi mwa Saudia.

Ingawa taarifa hiyo haikutaja moja kwa moja misikiti miwili mitakatifu ya Makka au Madina lakini sio kawaida kwa upigaji picha au utangazaji kufanyika katika msikiti mwingine wowote nchini Saudi Arabia, jambo ambalo liliibua maswali kuhusu msukumo wa awali wa tangazo hilo.

Wanaharakati kadhaa na watumiaji wa mitandao ya kijamii walikuwa wamekosoa hatua ya kupiga marufuku matangazo ya umma ya maombi.

"Kufuatia mialiko ya Nicki Minaj, sherehe za 'Giant' za jangwani, fukwe za bikini, kutoa elimu ya Kiislamu kutoka kwa mitaala, na kupiga marufuku vipaza sauti misikitini, #SaudiArabia [Mrithi wa Kiti cha Ufalme, Mohammed] Bin Salman amepiga marufuku vyombo vyote vya habari kutangaza Sala katika mwezi wa Ramadhani," aliandika mchambuzi wa Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) Sami Hamdi, akimaanisha mipango kadhaa ya hivi majuzi yenye utata katika ufalme huo.

Hamdi alichapisha taarifa na kusema kuwa huo ulikuwa mfano mwingine wa Saudi Arabia wa makusudi wa kuchapisha taarifa isiyoeleweka, kisha kutathmini upinzani, kabla ya kubatilisha.

Alitoa mfano wa mwanzoni mwa mwaka huu, wakati ufalme huo ulipozuia matumizi ya vipaza sauti vya nje katika misikiti, kabla ya kuthibitisha baadaye kwamba mafuruku hiyo ni ya wakati wa sala ya Ijumaa pekee.

"Je, una uhakika ni [Wizara ya] Masuala ya Kiislamu, au ni Wizara ya Vita vya Msalaba?!" alisema mtumiaji mwingine wa Twitter.

Baadhi ya wakosoaji wanaamini kuwa wakati wa Mohammed bin Salman ambayo kimsingi ndiye mtawala mkuu wa Saudi Arabia nchi hiyo imezidi kujitenga na kanuni za Uislamu ambao umekuwa ukifuatwa katika ufalme huo..

Mnamo Desemba, ufalme huo ulikosolewa na wahafidhina baada ya kuandaa tamasha la muziki la MDL Beast, ambalo lilishuhudia mamia ya maelfu ya wanaume na wanawake wakicheza pamoja. Utawala wa Saudia umekuwa ukitumia mkono wa chuma na ukatili dhidi ya wapinzani ambapo hivi karibuni makumi ya wapinzani walinyongwa.

3478266

Kishikizo: makka madina
captcha