IQNA

Mufti wa Misri

Wenye misimamo mikali hutoa Fatwa zitokanazo na ufahamu mbovu wa Qur'ani

19:19 - December 19, 2021
Habari ID: 3474696
TEHRAN (IQNA)- Mufti Mkuu wa Misri amesema Fatwa nyingi ambazo hutolewa na wale wenye misimamo mikali nay a kufurutu ada na ambazo huharibu sura ya Uislamu halisi hutokana na ufahamu mbovu wa Qur'ani Tukufu.

Sheikh Shawki Allam amebainisha masikitiko yake kuwa Fatwa kama hizo husababisha matatizo kama vile mauaji na uharibifu.

Ameongeza kuwa , kuna wakati mmoja ambapo ufahamu usio sahihi wa Qur'ani Tukufu ulipelekea Misri kupotea mkondo. Amesema makundi ya kigaidi hayajaweza kufahamu maana halisi ya aya za Qur'ani na Hadithi za Mtume Muhammad SAW.

Sheikh Allam amebainisha masikitiko yake kuwa, Fatwa kama hizo potovu zimepelekea sura nzuri ya Uislamu kuharibika duniani.

4022000

captcha