IQNA

Wamarekani walaani misimamo ya Facebook dhidi ya Uislamu

17:16 - November 16, 2021
Habari ID: 3474564
TEHRAN (IQNA) – Mamia ya watu kutoka dini mbali mbali wamekusanyika katika miji kadhaa mikubwa Marekani kulaani hatua ya Facebook kuruhusu matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu nchini India.

Waandamanaji wamebainisha hasira zao kuhusu hatua ya Facebook kuruhusu jukwaa hilo la mtandao wa kijamii kutumiwa kueneza taarifa za kichochezi nchini India ambazo zimepelekea kushambuliwa na kuuawa Waislamu na watu wengine wajamii za waliowachache.

Maandamano hayo yameratibiwa na Taasisi ya Kuangazia Maangamizi ya Kimbari India na walioshiriki wamemtaka mkurugenzi mkuu na muasisi wa Facebook, Mark Zuckerberg kusitisha sera ya sharia lake ya kuunga mkono wahindu wenye misimamo ya kufurutu ada.

Maandamano yamefanyika Atlanta, Chicago, Charlotte, Houston, Los Angeles, San Diego, Seattle na San Francisco katika katika eneo la Menlo Park ambalo yako makao makuu ya Facebook.

Waandamanaji wengi walioshiriki wana asili ya India lakini hawawezi kurejea India kutokana na hofu kuhusu kukabiliwa na mashambulizi yanayoungwa mkono na serikali.

Hivi karibuni ilifichuliwa kuwa Facebook nchini India imekuwa ikiacha kwa makusudi taarifa za chuku dhidi ya Waislamu zienezwe.

Nyaraka zilizofichua uovu huo wa Facebook zimevujiswa na Frances Haugen, ambaye alikuwa mfanyakazi wa Facebook. Haugen anasema Facebook ilikuwa inafahamu kuhusu tatizo hilo la taarifa za chuku lakini ilikataa kuchukua hatua.

3476507

Kishikizo: facebook india waislamu
captcha