IQNA

Nasrallah: Mazoezi kijeshi ya Israel ni ishara wasiwasi wake mkabala wa Lebanon

12:24 - November 12, 2021
Habari ID: 3474544
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, mazoezi kijeshi yanayofanywa mara kwa mara ya na utawala haramu wa Israel ni kielelezo cha wasiwasi na woga wa utawala huo mkabala wa Lebanon

Katika hotuba yake ya jana iliyotolewa kwa mnasaba wa Siku ya Shahidi, Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, mazoezi hayo ya kijeshi yanaonesha kuwa Israel ina hofu kwamba Lebanon inaweza kushambulia makoloni ya utawala huo huko al Jalil na kwa sababu hilo kila mwezi inafanya mazoezi ya kijeshi katika eneo hilo.

Sayyid Nasrallah amesema, utawala haramu wa Israel unataka kutimiza njama zake kupitia njia ya kuanzisha uhusiano na nchi za Kiarabu. Amesisitiza kuwa nchi zinazoanzisha uhusiano na utawala huo ghasibu haziwezi kulinda usalama wa Israel.    

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa nchi za Kiarabu hatimaye zimekiri kwamba Syria imeibuka na ushindi.

Amasema mashahidi walikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa Muqawama dhidi ya njama ya kigaidi ya Marekani eneo la Magharibi mwa Asia na kuongeza kuwa: Katika siku za karibuni kumeripotiwa habari za mamasiliano ya baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu na Rais Bashar Assad wa Syria, suala ambalo ni sawa na kukubali na kukiri ushindi wa serikali ya Damascus, na vilevile kukiri kwamba mradi wa nchi za Kiarabu uliogharimu mabilioni ya dola, umefeli. 

Sayyid Nasrallah amesema, utawala haramu wa Israel unataka kutimiza njama zake kupitia njia ya kuanzisha uhusiano na nchi za Kiarabu. Amesisitiza kuwa nchi zinazoanzisha uhusiano na utawala huo ghasibu haziwezi kulinda usalama wa Israel.    

4012437

captcha