Hivi sasa kufuatia kupungua maambukizi ya COVID-19 na pia kupungua kwa kiwango kikubwa idadi ya wanaopoteza maisha kutokana na ugonjwa, huo, Kamati Kuu ya Kukabiliana na COVID-19 imetangaza kuwa misikiti itaruhusiwa kuwa na Sala ya Ijumaa kuanzia Septemba 24.
Idhini hiyo hiyo imetolewa kwa masharti ambapo wale tu waliopata chanjo ya COVID-19 ndio watakaoruhusiwa kushiriki katika Sala ya Ijumaa. Aidha wanaosiriki katika Sala ya Ijumaa wanatakiwa kuzingatia kanuni za kukabiliana na COVID-19 kama vile kutokaribiana, kila moja kubeba mkeka binafsi wa kusali, kuvaa barakoa na wanaosalia msikiti wasizidi asilimia 50 ya idadi inayoruhusiwa.