Mtukufu huyo alipewa jina la 'Jawad' likiwa na maana ya mtu mkarimu sana kutokana na ukarimu wake mkubwa. Imam Jawad alizaliwa katika mwezi wa Ramadhani mwaka 195 Hijria na kuongoza Umma wa Kiislamu baada ya kuuawa shahidi baba yake, Imam Ridha AS. Aliuawa shahidi akiwa na umri wa miaka 25 na amezikwa pembizoni mwa babu yake, Imam Musa Kadhim AS katika eneo la Kadhimiya kaskazini mwa Baghdad.