IQNA

Hizbullah yalaani uamuzi wa Marekani kuteka tovuti za mrengo wa muqawama

11:42 - June 25, 2021
Habari ID: 3474040
TEHRAN (IQNA) - Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali hatua ya serikali ya Marekani kuteka na kufunga tovuti kadhaa za vyombo vya habari vya Iran na kieneo na kusema kitendo hicho ni jinai inayothibitisha sera za ukandamizaji zinazfuatwa na Washington.

Mkuu wa Ofisi ya Mahusiano ya Umma ya Hizbullah Mohammad Afif amesema kitendo hicho kiovu cha Marekani kinalenga kuficha ukweli kuhusu jinai ambazo imezitenda pamoja na waitifakki wake dhidi  watu wanaodhulumiwa katika eneo hasa watu wa Yemen na Palestina ambao wanakabiliwa na mzingiro mbaya zaidi.

Naye Qais Khazali, kiongozi wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya Iraq amelaani hatua ya Marekani kufunga tovuti za habari za Iran na harakati za muqawama katika eneo. Amesema kitendo hicho kinaweza wazi ukweli kuwa nchi za Magharibi zinahadaa zinapodai kutetea haki za binadamu na uhuru wa maoni. Amesema Marekani imeteka tovuti za habari ambazo zimekuwa zikipinga njama za Marekani, Uingereza, utawala wa Israel, Saudia na Imarati. Amesema kitendo hicho cha Marekani ni ithbati tosha kuwa imeshindw akijeshi na sasa imeamua kukpambana na fikra.

Juzi serikali mpya ya Marekani iliendeleza sera za kiijuba ya kibeberu za nchi hiyo kwa kuzifunga tovuti za televisheni za kimataifa za Iran na vyombo vya habari vya mrengo wa muqawama au mapambano ya Kiislamu Yemen, Palestina, Iraq na Bahrain.

Televisheni ya Kiingereza ya Iran ya Press TV na zile za Kiarabu za Al Alam na Al Khauthar ni kati ya vyombo vya habari ambavyo vimefunguiwa tovuti zao na Marekani.

Kufuatia hatua hiyo Press TV imetangaza kuwa tovuti iliyofungwa ya presstv.com  sasa inapatikana kupitia presstv.ir

/3979838

captcha