IQNA

Wapalestina 40,000 washiriki Sala ya Ijumaa Al Aqsa

22:18 - May 29, 2021
Habari ID: 3473959
TEHRAN (IQNA)- Sala ya Ijumaa imeswaliwa jana katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) ambapo inakadiriwa kuwa Wapalestina 40,000 walishiriki katika sala hiyo.

Wapalestina waliweza kufika katika msikiti huo pamoja na kuwepo ivingiti vingi vilivyowekwa na utawala ghasibu wa Israel ili kuwazuia Waislamu kuswali Sala ya Ijumaa hapo.

Sheikh Azzam Khatib, mkurugenzi mkuu wa  Idara ya Wakfu ya Jordan inayosimamia Msikiti wa Al Aqsa, idadi kubwa ya waumini walifika msikitini hapo mapema Ijumaa asubuhi.

Siku ya Alhamisi, ikiwa ni katika kuendeleza uchokozi wao, mamia ya walowezi wa Kizayuni waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuuvunjia heshima wakiwa wanalindwa na askari wa utawala haramu wa Israel. Mamlaka ya Ndani ya Palestina imelaani vikali vitendo hivyo na kusema vinalenga kuvuruga mapatano ya usitishwaji vita yaliyofikiwa baina ya harakati za muqawama Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.

3974181

 
 
captcha