IQNA

Utawala wa Kizayuni wadondosha mabomu katika Ukanda wa Ghaza

22:14 - August 18, 2020
Habari ID: 3473080
TEHRAN (IQNA) - Ndege za kivita za utawala haramu wa Kizayuni leo asubuhi zimeshambulia ngome za harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) katika Ukanda wa Ghaza.

Msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni amesema kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa kutumwa katika vitongoji vya Wazayuni maputo ya moto kutokea Ukanda wa Ghaza. 

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana usiku pia zilishambulia eneo la al Brij huko katikati mwa Ghaza.

Vijana wa Kipalestina siku kadhaa za karibuni walirusha vishada vya moto katiak ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu  wakilalamikia kuendelea kuzingirwa Ukanda wa Ghaza na Wazayuni.  

Ndege za kivita, helikopta, na makombora ya utawala wa Kizayuni katika miezi ya karibuni ziliyashambulia kwa mara kadhaa maeneo mbalimbali huko Ghaza. 

3472320

captcha