Kwa mujibu wa taarifa, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Palestina imesema kwa sasa ni Swala ya Ijumaa tu utakayorushusiwa na marufuku ya swala za jamaa misikitini itaendelea hadi uamuzi utakapochukuliwa.
Wiki iliyopita, Wizara ya Wakfu ya Palestina iliruhusi Swala ya Ijumaa na pia Swala ya Idul Fitr kwa kuzingatia kanuni maalumu za afya katika misikiti. Kati ya kanuni hizo ni watu kutokaribiana wakati wa swala, kutopeana mikono na kila muumini kuja msikini na mkeka wake binafsi wa kuswalia.
Wizara ya Afya ya Palestina inasema hadi kufikia sasa walioambukizwa corona katika Ukanda wa Ghaza ni 61.