IQNA

Maulamaa wa Mapambano ya Kiislamu wakutana Iraq kujadili 'muamala wa karne'

10:58 - February 23, 2020
Habari ID: 3472497
TEHRAN (IQNA) – Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu wamekutana, Baghdad, Iraq jana Jumamosi.

Maudhui huu katika mkutano huo ilikuwa ni 'Umoja wa Iraq, Mamlaka ya Kujitawala na Ushindi kwa Palestina na Umma wa Kiislamu."

Washiriki katika kongamano hili waliafikiana kwa kauli moja kuhusu kupunga 'muamala wa karne' uliopendekezwa na Marekani kuhusu Palestina.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iraq, Ayatullah Sayyed Mojtaba Husseini alisisitiza kuhusu kuwa macho mbele ya njama za adui na kupinga dhulma na udikteta.

Aidha alisema kadhia ya Palestina ni maudhui muhimu zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu na ni mhimili wa umoja wa Waislamu.

Akihutubia kikao hicho, mwanazuoni mwandamizi wa Kisunni nchini Iraq Sheikh Abdul Latij al Humaim alisema Mji wa Quds (Jerusalem) ni nembo ya utmabulisho wa Kiislamu. Naye balozi wa Palestina nchini Iraq Ahmed Aql alilaani mpango wa 'muamala wa karne' na kusema rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu hawatapata chochote katika muamala huo.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Jumanne ya tarehe 28 Januari, Rais wa Marekani, Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizindua mpango wa Muamala wa Karne katika Ikulu ya White House.

Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.  

Mpango huo umepingwa vikali kote duniani na hata ndani ya Marekani kwenyewe.

3470716

captcha