Mkuu wa kitengo cha Bidhaa Halali katika Idara ya Ustawi wa Kiislamu Malaysia Dkt. Sirajuddin Suhaimee anasema kumekuwepo na ongezko kubwa la ununuzi wa bidhaa halali si tu kutoka nchi za Kiislamu bali hata kutoka nchi zisizo za Kiislamu ambazo zinataka bidhaa na huduma halali.
Amesema kati ya nchi zisizo za Kiislamu ambazo zinataka bidhaa zenye cheti cha Jakim ni pamoja na China, Japan, Taiwan na Hong Kong. Sirajuddin anasema mashirika ya kimataifa ambayo yanataka cheti cha 'Halal' cha Jakim huchukua miezi mitatu kupata cheti hicho. Aidha amesema hivi sasa nchi 42 duniani zimeafiki cheti cha 'Halal' cha Jakim ambapo za hivi karibuni kabisa zilikuwa ni Lithuania na Kazakhstan.
3466622