Ndugu hao watatu, wawili wa kiume na moja wa kike kutoka mkoa wa Beni Suef, wameweza kuhifadhi kikamilifu na hivyo kuthibitisha kuwa sahihi ule msema usemao kuwa ‘Ulemavu sio ukosefu wa uwezo.’
Moja kati ya watoto hao wenye ulemavu wa macho ambaye yuko katika shule ya msingi anasema: “Kila wakati ninapotoka shuleni na kurejea nyumbani, hujishughulisha na kuhifadhi Qur’ani na kusikiliza tilawa ya aya za Qur’ani.”
Anasema wazazi wake wamempa motisha sana na ni moja ya sababu za mafanikio yake katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.
Baba mzazi wa watoto hao watatu wenye ulemavu wa machi anasema: “Qur’ani Tukufu inamjenga mwanadamu name nimejaza mahaba ya Qur’ani katika nyoyo za watoto wangu tokea wakiwa wachanga.”
Wakati huyo huo shirika moja la misaada Misri limetangaza mpango wa kuwasaidia watoto hao wafanyiwe upasuaji ili kuboresha uwezo wa macho yao. Kwa maelezo zaidi sikiliza au tizama klipu ya video inayofuata hapa chini.