Mshindi wa mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu alikuwa ni Hadil Khalid wa Palestina ambaye alipata zawadi ya Dirhamu 250,000. Ramla Hassan wa Finland alishika nafasi ya pili na kupata zawadi Dirhamu 200,000, huku Israa Husam wa Bahrain na Noura Muhammad Ahmad wa Marekani wakishika nafasi ya tatu kwa pamoja na hivyo kila moja wao akipata zawadi ya Dihramu 150,000.
Washindi wa kitengo cha 'usomaji maridadi zaidi' walikuwa Salma Mohammad wa Morocco huku nafasi ya pili ikishikwa na Zakia Juma Ramadhan wa Tanzania na Reem Monther wa Jordan.
3464506