IQNA

Iran yaandaa maonyesho ya Qur'ani nchini Sierra Leone

12:29 - September 15, 2016
Habari ID: 3470564
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa maonyesho ya Qur'ani Tukufu nchini Sierra Leone magharibi mwa Afrika.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yaliyopewa anuani ya 'Qurani Tukufu na Sayansi za Qur'ani kwa Mtazamo wa Sanaa' yameandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown.

Maoneysho hayo ya siku tano yalifunguliwa hiyo juzu katika sherehe iliyohudhuriwa na Sheikh Ahmad Tejani Sila, Kiongozi wa Mashia wa Sierra Leone pamoja na maulmaa, maimamu, wanafunzi na watu wa matabaka mbali mbali.

Washiriki katika maonyesho hayo wamesisitiza kuhusu umuhimu wa kutumia athari za Sanaa za Qur'ani katika kufikisha ujumbe wa kitabu hicho kitukufu. Akizungumza katika kikao hicho, Mwambata wa Utamduni wa Iran nchini Sierra Leone Bw. Mohamad Maarefat amesema lengo la kuandaa maonyesho hayo ni kuwakumbusha watu kuhusu Mwezi wa Dhil Hijja na utekelezaji Ibada ya Hija kwa msingi wa Qur'ani Tukufu.

Katika maonyesho hayo kulikuwa na athari kadhaa za tarjama na tafsiri za Qur;ani Tukufu na pia nakala za Qur'ani zilizoandikwa kwa kaligrafia. Halikadhalika washiriki wa maonyesho hayo walikabidhiwa ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Waislamu duniani katika munasaba wa Ibada ya Hija mwaka huu.

Sierra Leone ni nchi iliyo maghairbi mwa Afrika na ina idadi ya watu milioni 7 ambapo zaidi ya wakaazi asilimia 78.0 ni Waislamu.

Iran yaandaa maonyesho ya Qur'ani nchini Sierra LeoneIran yaandaa maonyesho ya Qur'ani nchini Sierra LeoneIran yaandaa maonyesho ya Qur'ani nchini Sierra Leone

3530047

Kishikizo: iqna qurani sierra leone
captcha