IQNA

Mafunzo ya Qur'an kwa watoto Visiwa vya Comoro

18:08 - April 09, 2016
Habari ID: 3470235
Mafunzo ya maalumu kuhifadhi na kusoma (tajwid) Qur'an Tukufu yamefanyika katika Visiwa vya Comoro kwa kuhudhuriwa nawanafunzi takribani 100.
Kozi hiyo fupi ya mafunzo ya Qur'an ilifanyika kwa muda wa siku 50 na kusimamiwa na Jumuiya  ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'an kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo ya kuhifadhi na kusoma Qur'an cha Sa'd ibn Mu'adh.
Mwishoni mwa duru hiyo, kulifanyika hafla kubwa iliyohudhuriwa na walimu na wasomi wa dini ya Kiislamu wanaojihusisha na shughuli za kufundisha kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu, ambapo pia washiriki walipewa zawadi mbalimbali.
Msemaji wa kozi hiyo hiyo sambamba na kusisitizia umuhimu wa kufundishwa watoto Qur'an Tukufu, alitoa shukurani za dhati kwa jitihada za Jumuiya  ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani katika kueneza utamaduni wa Qur'ani kote duniani. Visiwa vya Comoro ambavyo pia vinajulikana kama Ngazija vinapatikana eneo la kusini mashariki mwa bara la Afrika katika Bahari ya Hindi. Nchi hiyo ni mwanachama wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Arab League na pia Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC.
3486617
Kishikizo: ngazija comoro
captcha