IQNA

Mufti Mkuu wa Quds

Watawala wa Israel wachukuliwe hatua

16:18 - July 27, 2015
Habari ID: 3335935
Mufti Mkuu wa Palestina ametoa wito wa kuhukumiwa wakuu wa wutawala wa Kizayuni wa Israel katika duru za kimataifa.

Sheikh Muhammad Hussein amelaani hatua zinazochukuliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na kusema kuendelea kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu huko Quds hususan Msikiti wa al Aqsa kutalitumbukiza eneo la Mashariki ya Kati katika ghasia na machafuko.
Sheikh Muhammad Hussein amesema walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakihamasishwa kuvunjia heshima na kushambulia Msikiti wa al Aqsa. Mufti wa Quds pia ameutaka Umma wa Kiislamu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Kamati ya Quds kuingilia kati haraka iwezekanavyo na kusitisha jinai zinazofanywa na utawala katili wa Israel.
Wakati huo huo katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu na Kikristo ya Kulinda Quds Tukufu Hana Isa ametahadharisha kuhusu njama zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na mashambulizi ya askari wa Israel dhidi ya watu wanaotekeleza ibada ya Swala katika msikiti huo.../mh

3335616

captcha