IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu kufanyika Uingereza

11:03 - August 17, 2014
Habari ID: 1439998
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Uingereza yamepangwa kufanyika mwezi ujao nchini humo yakiwashirikisha vijana wa Kiislamu.

Mwandishi wa IQNA nchini Uinereza amenukuu mtandao wa QuranFocus kwamba mashindano ya 19 ya Qur'ani Tukufu yatafanyika Jumapili tarehe 7 Septemba katika kitengo cha hifdhi ya Qur'ani Tukufu.
Taasisi ya Kiislamu ya al Birr ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambayo lengo lake ni kuwahamasisha vijana wa Kiislamu wa Uingereza kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Washindi katika mashindano hayo watatunukiwa zawadi za hadi pauni elfu 5 na shahada ya kushiriki kwenye zoezi hilo.
Mashindano hayo yatawashirikisha vijana wenye umri wa chini ya miaka 22.

1438070

captcha