IQNA

Bunge la Misri lajadili pendekezo la tafsiri mpya ya Qur’ani Tukufu

20:56 - December 22, 2021
Habari ID: 3474707
TEHRAN (IQNA)- Kamati ya Kidini katika Bunge la Misri limeanza kujadili pendekezo la kuandika tafsiri mpya ya Qur’ani Tukufu.

Yusuf Sayyid Amer, mwenyekiti wa kamati hiyo amewasilisha pendekezo  hilo ili lijadiliwe bungeni.

Ameongeza kuwa tafsiri mpya ya Qur’ani itakayotayarishwa itazingatia misimamo ya wastani katika Uislamu na kuwasilisha muelekeo wenye kukabiliana na misimamo mikali.

Halikadhalika amesema tafsiri hiyo italenga kujibu maswali kuhusu Hadithi ambazo makundi  yenye misimamo mikali hutumia katika kutetea misimamo yao mikali ya kidini, amesema Amer.

Wazri wa Wakfu Misri Sheikh  Mukhtar Gomaa ambaye alishiriki katika kikao hicho amesema  kadiri muda unavyosonga mbele kuna haja ya kuwa na tafsiri mpya za Qur’ani Tukufu.

Aidha anasema kuna mkakati wa kuhakikisha kuwa mafunzo ya kidini yanapatikana  kwa lugha yenye kufahamika na waliowengi katika jamii.

4022590

captcha