IQNA

Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS yafanyika Lamu, Kenya

21:09 - September 28, 2021
Habari ID: 3474356
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika eneo la Matondoni, kaunti ya Lamu nchini Kenya leo wameshiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Mjumuiko huo umeongozwa na msomi maarufu wa Kiislamu Afrika Mashariki Sheikh Sayyid Aidarus Shariff Alwy - Mzee Mwenye

Maadhimisho siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

 
Kishikizo: arubaini lamu Aidarus
captcha