IQNA

Tehran mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu

18:39 - December 13, 2016
Habari ID: 3470739
IQNA-Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema mkutano wa kimataifa wa kila mwaka wa umoja wa Kiislamu utafanyika wiki hii mjini Tehran.

Kwa Mujibu wa Ayatullah Muhsin Araki, mkutano huo ni nembo ya Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu katika kukabiliana na maadui.

Akizungumza Jumanne mjini Tehran, Ayatullah Araki amesema mkutano huo utaanza Alhamisi na kuendelea kwa muda wa siku tatu na kuwaleta pamoja wasomi na wanaharakati wa Kiislamu kutoka nchi zaidi ya 50. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema mwaka kuna vikao vya umoja wa Kiislamu kote Iran na maeneo mengine duniani katika Wiki wa Umoja. Aidha amesema sherehe za Miladun Un Nabii na Wiki ya Umoja wa Waislamu mwaka huu ni bora zaidi ya miaka iliyopita na hili linaonyesha kuimarika umoja wa Kiislamu.

Ayatullah Muhsin Araki amesema maudhui ya umoja na udharura wa kukabiliana na wimbi la ukufurishaji ni mihiili miwili muhimu ya mkutnao ya kimataifa ya Kiislamu wa Tehran mwaka huu. Amesema mkutnao huo utahudhuriwa na wasomi 320 wa kitaifa na kimataifa huku akibainia kuwa magaidi wanaelekea kufeli katika njama yao ya kuanzisha vita vya kimadhehebu baina ya nchi za Kiislamu.

Kwa kauli ya Ahul SunnaMtume Muhammad SAW rehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal hukuWanachuoni wa madhehebu ya Shia wakiamini alizaliwa tarehe 17 Rabiul Awwal mwaka huohuo. Kwa msingi huo, Imam Khomeini, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.

captcha