IQNA

Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake

Hongera kwa munasaba wa kuanza mwezi wa Rabiul Awwal, machipuo ya uhai
Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake
"Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake." Al Baqara/207
Ayah hii tukufu iliteremshwa katika usiku wa tarehe Mosi Mfungo Sita, Rabiul Awwal kwa ajili ya Amir ul Muminin Ali AS.
Katika usiku huo, Mtume SAW aligura kutoka Makka kuelekea Madina kwa ajili ya kuepuka shari ya makafiri.
Imam Ali AS, ambaye amebakia shujaa katika historia, aliweka maisha yake hatarini na kulala katika kitanda cha Rasulullah SAW. Usiku huo ulikuwa usiku ujulikanao kama Laylat al-Mabit…
Imam Ghazali katika kitabu chake cha Ihya'ul ulumuddin anasema:
Katika usiku ambao, Amirul Muminin Ali AS alilala katika kitanda cha Mtume SAW, Malaika Jibril na Mikail walipokea ujumbe kuwa, 'mimi nimeleta udugu baina yenu nyinyi wawili na nimeweka umri wa moja wenu kuwa zaidi ya mwingine. Ni yupi baina yenu atajitolea ili umri wa mwenzake uwe mrefu zaidi?
Wote wawili wakachagua umri mrefu. Hapo ukaja ujumbe ufuatao: "Tizameni katika ardhi muone ni vipi Imam Ali AS ametoa umri wake kwa ajili ya nduguye, Mtume Mtukufu SAW, na akalala katika kitanda chake na kwa njia hiyo akaitoa muhanga roho yake kwa ajili ya Mtume SAW. Nendeni katika ardhi na mumuokoe kutoka katika shari ya maadui."
Wakashuka katika ardhi na Jibril akakaa pembeni mwa kichwa cha Amirul Muuminin naye Mikail akaenda upande wa miguu ya mtukufu huyo na kusema: "Ni nani kama wewe, Ewe Abi Talib, Mwenyezi Mungi amejifakahrisha kwako mbele ya Malaika. Hapo aya Tukufu ya:
" Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu…" ikashuka.
Ihya'ul ulumuddin-Ghazali, Kitabu cha 7  kuhusu Kujitolea Muhanga Nafsi