IQNA

Waislamu washiriki katika maombolezo ya Bwana Mtume SAW

21:28 - November 28, 2016
Habari ID: 3470703
IQNA-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana usiku na leo imeghariki kwenye huzuni na majonzi kwa kukumbuka siku aliyoaga dunia Bwana Mtume Muhammad SAW na aliyokufa shahidi Imam Hassan Al-Mujtaba AS.

Hafla za maombolezo zilifanyika nchini kote katika misikiti, husaniyyah na maeneo mengine matakatifu ya kidini na zinaendelea pia hii leo kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyofariki dunia mbora huyo wa viumbe na mjukuu wake kipenzi.

Hafla za maombolezo kwa mnasaba huo zimefanyika pia katika nchi na maeneo mbalimbali duniani.

Nchini Uingereza mamia ya Waislamu na wapenzi wa Ahlul Bayt (AS) jana usiku walishiriki kwenye halfa ya maombolezo hayo iliyofanyika katika kituo cha Kiislamu mjini London.

Hafla hiyo ya maombolezo ilihudhuriwa na Wairan wanaoishi mjini London pamoja na Waislamu wa mataifa mengine.

Katka hafla hiyo Hujjatul Islam Issa Jahangir alizungumzia shakhsia ya Bwana Mtume Muhammad SAW na kueleza kwamba kutokana na kupambika kwa akhlaqi njema na mantiki imara, mtukufu huyo alifanikiwa kutekeleza jukumu la kufikisha ujumbe wa Allah na kuyashinda matatizo na masuala mbalimbali aliyokabiliana nayo.

Ameongeza kuwa kuamiliana kiadilifu na kwa njia sahihi na watu, kuchanganyika na watu, kutopenda makuu na kukataa kusifiwa ni miongoni mwa sifa nyingine muhimu zilizopambashakhsia yenye nuru, na kushuhudiwa katika tabia na mwenendo wa Bwana Mtume SAW.

Kwa mnasaba wa kukumbuka kuaga dunia Mtume mtukufu Muhammad Al-Mustafa SAW pamoja na kufa shahidiImam Hassan Al-Mujtaba AS na Imam Ali Ibn Mussa Ridha AS, hafla za maombolezo kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifarsi zinafanyika kwa muda wa siku tatu katika kituo cha Kiislamu mjini London, Uingereza.

Mwezi 28 Mfunguo Tano Safar, inasadifiana na siku ya kukumbuka alipofariki dunia Bwana Mtume Muhammad SAW na pia ni siku aliyouawa shahidi mjukuu wake, Imam Hassan AS.



3461538
captcha