IQNA

Iran yakosoa madai yasiyo na msingi ya Saudia

11:09 - September 03, 2016
Habari ID: 3470546
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa madai yasiyo na msingi ya Saudi Arabia dhidi yake na kutoa wito kwa watawala wa Riyadh kutoruhusu 'ndoto' kutawala vitendo vyao Mashariki ya Kati.

Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi amesema Saudi Arabia inapaswa kutafakari kwa kina kuhusu kubadilisha tabia zake katika eneo na katika uga wa kimataifa.

Qassemi ametoa kauli hiyo kujibu tuhuma zisizo na msingi ambazo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al-Jubeir dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza katika mji mkuu wa Japan, Tokyo siku ya Ijumaa, al Jubeil alidai kuwa eti Iran inahusika na vitendo vya 'hujuma' Mashariki ya Kati. Siku ya Jumatano pia alitoa tuhuma kama hizo akiwa katika mji mkuu wa China.

Akijibu tuhuma hizo Qassemi ameyataja kuwa yasiyo na msingi wowote madai ya Adel al Jubeir na maafisa wengine wa Saudia dhidi ya Iran. Jubeir ambaye ana historia ndefu ya kutoa madai ya kipuuzi dhidi ya Iran alisema eti Tehran inapelekea silaha Bahrain, Kuwait na  Saudia. Qassemi amesema Iran inatoa msaada wa kimaanawi na kisiasa kwa Wasyria na watu wa baadhi ya nchi za Kiislamu katika eneo ambao wanalengwa na makundi ya magaidi wakufurishaji.

Siku ya Alhamisi pia Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema Saudi Arabia ni chanzo cha ugaidi na itikadi kali za Kiwahhabi duniani. Aliongeza kuwa Saudia imefeli katika jitihada zake za kujaribu kufunika maovu yake duniani.

352724

captcha