IQNA – Waziri wa Elimu wa Misri amesisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano imara kati ya wanafunzi na Qur’ani tangu miaka ya mwanzo ya elimu.
Mohamed Abdel-Latif ametoa wito wa kuzingatia maadili ya kielimu na kimaadili sambamba na kufundisha masomo ya msingi, na akasisitiza umuhimu wa kuhifadhi angalau Juzuu mbili za Qur’ani Tukufu katika kipindi chote cha miaka sita ya shule ya msingi nchini humo.
Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha nafasi ya elimu ya dini mashuleni na haja ya kuzingatia kuhifadhi Qur’ani Tukufu kwa wanafunzi wa shule za msingi.
Hatua hii ni sehemu ya ahadi pana ya kujenga haiba na kukuza maadili na kanuni, sambamba na mafanikio ya kitaaluma, alisema.
Abdel-Latif alibainisha kuwa kuhifadhi aya za Qur’ani ni jambo la kusifiwa na linawasaidia watoto na wanafunzi kukuza ustadi wa lugha ya Kiarabu, na akaonyesha matumaini kwamba kiwango hiki kitaongezeka.
Aliongeza kuwa huu si uamuzi mpya, kwani mtaala huu umewekwa tangu mwaka uliopita wa masomo wa 2025-2026.
Waziri wa Elimu wa Misri ameagiza kuwa somo la “Elimu ya Dini” lifundishwe mashuleni. Agizo hili linataka ratiba ya shule ipangwe kwa namna ambayo wanafunzi watapata somo lao la elimu ya dini mwanzoni mwa siku ya shule, na siyo kuliahirisha hadi saa za mwisho; hivyo, huku ikiongeza manufaa yaliyokusudiwa ya somo hili, mahudhurio bora na ushiriki wa wanafunzi pia unahakikishwa.
Miongozo hiyo ilisisitiza umuhimu wa kuichukulia elimu ya dini kama sehemu muhimu ya mfumo wa maendeleo ya mwanafunzi unaojumuisha maadili, misingi ya kimaadili, na tabia chanya, badala ya kuichukulia kama maarifa yanayohusiana na maudhui ya kitaaluma pekee.
3498692