IQNA

Mafunzo ya kuokoa maisha katika misikiti Pakistan

11:28 - September 25, 2021
Habari ID: 3474339
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Madaktari wa Kiislamu Pakistan (PIMA) inapanga kuandaa warsha za kuokoa maisha kwa wananchi katika misikiti kote Pakistan.

Lengo la warsha hiyo limetajwa kuwa ni kutoa mafunzo kwa wananchi katika kuokoa maisha ili waweze kuwasaidia wale ambao wanakumbwa na mshtuko wa moyo n.k hasa katika maeneo ambayo hakuna suhula za kimsingi za kuokoa maisha.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa PIMA, Dkt. Khubaib Shahid, misikiti 189 imeteuliwa kushiriki katika warship hizo za ‘Mafunzo ya Kimsingi ya Kuokoa Maisha (BLS). Amesema idadi kubwa ya watu hupata mshtuko wa moyo kazini, nyumbani au maeneo ya ibada ambapo baadhi hupoteza maisha kutokana na wengi kutojua mbinu za kimsingi za kuokoa maisha.

3475777

Kishikizo: pakistan waislamu moyo
captcha