IQNA

Msikiti mkongwe zaidi India wafunguliwa tena

21:46 - September 23, 2021
Habari ID: 3474331
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kwanza na mkongwe zaidi nchini India unatazamiwa kufunguliwa tena baada ya kurejea katika hadhi na adhama yake ya awali.

Msikiti huo ambao ni maarufu kama ‘Cheraman Juma Masjid’ ulijengwa mwaka 629 Miladia (CE) na sasa umerejea katika hali yake ya kawaida kufuatia oparesheni ya kuukarabati ambayo imefanyika kwa muda wa miezi 30 kwa usimamizi wa taasisi ya kiserikali ya  ‘Mradi wa Turathi wa Muziris’.

Inasimuliwa kuwa msikiti huo ulijengwa na Malik Deenar, aliyekuwa ametoka Uajemi (Iran ya leo) kwa amri ya mfalme

Msikiti huo uko katika eneo la Kodungallur Taluk kati mwa jimbo la Kerala. Mbali na kukarabatiwa, pia katika karibu na msikiti huo kumejengwa Jengo la Makumbusho ya Turathi za Kiislamu wa Chera (Kerala ya leo).

Msikiti huo uliharibiwa na Warekani mwaka 1504 Miladia na kisha baada ya hapo kukarabatiwa mara kadhaa.

3475761

captcha