IQNA

Maziko ya mwanazuoni wa Kiislamu Lebanon kufanyika Jumatatu

19:22 - September 05, 2021
Habari ID: 3474262
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Lebanonm Sheikh Abdul Amir Qabalan ambaye aliyefariki dunia Jumamosi anatazamiwa kuzikwa Jumatatu.

Marhum Sheikh Qabalan ambaye pia alikuwa Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini Lebanon alifariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kwa muda mrefu na atazikwa katika kijiji chake eneo la Jabal.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya Kimataifa ya Kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Sheikh Qabalan.

Katika ujumbe wake, Hujjatul-Islam walmuslimin Dr. Hamid Shahriari ametoa mkono wa pole kwa taifa la Lebanon kwa mnasaba wa kufariki dunia  mwanazuoni huyo.. 

Sehemu moja ya salamu za rambirambi za Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu imesema: Mwanazuoni huyo mwema ambaye alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wa mwanzo wa umoja wa Kiislamu na kukaribiana baina ya madhehebu za Waislamu ametumia sehemu kubwa ya umri wake katika kulinda njia ya Mwenyezi Mungu na kupambana na maadui wa dini ya Allah hususan Wazayuni maghasibu na vibaraka wao. 

Ujumbe huo umesema himaya kubwa ya Sheikh Abdul Amir Qabalan kwa Intifadha ya mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel itabakia hai daima katika fikra za wanamapambano katika njia ya Mwenyezi Mungu. 

3475634

captcha