IQNA

Watoto wa Palestina washiriki matembezi ya Qur'ani Tukufu huko Ghaza

19:08 - September 05, 2021
Habari ID: 3474261
TEHRAN (IQNA)- Taasisi ya Dar Al-Quran na Al-Sunnah ya Ukanda wa Ghaza zimefanya matembezi makubwa ya watoto wa Qur'ani katika kambi ya Nuseirat katikati mwa eneo hilo

Matembezi hayo yalishirikisha  watoto 700 wa Kipalestina ili kusisitiza umuhimu wa kufundisha watoto Quran.

Watoto hao walioshiriki ni wale ambao wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu au wamehifadhi nusu ya Qur’ani Tukufu.

Matembei hayo yalianzia  mbele ya Msikiti wa Al-Farouq hadi kufikia Mtaa wa Salahaddin ambapo watoto walitembea katika barabara za Kambi ya Nuseirat, wakiwa wamebeba Misahafu na mabango.

Katika hotuba baada ya kumalizika hafla hiyo, Abdul Rahman Al-Jamal, rais Taasisi ya Dar Al-Quran na Al-Sunnah ya Ukanda wa Ghaza, aliwashukuru washiriki wa matembezi  hayo.

Akisisitiza kuwa watoto walioshiriki katika matembezi hayo ni "kizazi cha ukombozi" ambacho kitakomboa Msikiti wa Al-Aqsa unaokaliwa kwa mabavu na Israeli mjini Quds (Jerusalem), Al-Jamal alisema kuwa maelfu ya watoto katika Ukanda wa Gaza wanafanya kila wawezalo kuhifadhi Qur’ani.

Al-Jamal pia aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kidini ili waweze kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

3995084

captcha