IQNA

Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Misri kufanyika Disemba

21:44 - August 02, 2021
Habari ID: 3474151
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Misri yatafanyika mwezi Disemba kama ilivyopangwa, amesema waziri wa wakfu nchini humo Sheikh Mokhtar Gomaa.

Aidha amesema wizara yake imetanga takribani dola za Kimarekani 63,618 kwa ajili ya zawadi za watakaoshinda katika mashindano hayo ambayo yatafanyika baina ya 11-15 Disemba.

Waziri Gomaa ameongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na kategoria za kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu kwa kuzingatia hukumu za tajweed na pia kategoria ya kuhifadhi na kubainisha maana ya aya kwa wazungumzao lugha ya Kiarabu. Halikadhalika kashindano hayo yatakuwa na vitengo vya wanawake na wanaume na washiriki hawapaswi kuwa zaidi ya umri wa miaka 35. Katika kategoria ya qiraa au kusoma Qur’ani Tukufu washiriki pia hawapaswi kuwa zaidi ya umri wa miaka 30.

Kategoria nyingine katika Mashindano ya 28 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Misri itakuwa ni ile ya watu wenye ulemavu na washiriki, ambao katika duru hii ni Wamisri pekee, hawapaswi kuwa zaidi ya umri wa miaka 30.

Washiriki wa kigeni watapokea mwaliko rasmi kutoka Wizara ya Wakfu ya Misri.

3987890

captcha