IQNA

Jeshi la Misri lasema limeua waasi 89 eneo la Sinai

22:09 - August 01, 2021
Habari ID: 3474147
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Misri lilisema Jumapili limewaua watu 89 wanaoshukiwa kuwa waasi katika operesheni Kaskazini mwa Sinai, mkoa ambao kundi la kigaidi linalofungamana na kundi la kigaidi la Daesh limekuwa likitekeleza hujuma.

"Kati ya juhudi zinazoendelea katika kutafuta na kuangamiza makundi kigaidi ... katika kipindi cha awali, vikosi vya jeshi ... vilifanya operesheni ambazo ziliua magaidi 89 hatari wakufurishaji ... kaskazini mwa Sinai," msemaji wa jeshi alisema.

Kauli yake, akitumia neno "wakufurishaji" kumaanisha waasi wenye itikadi kali za kidini, haikuainisha muda wa operesheni, lakini alisema jeshi lilipata majeruhi wanane.

Jeshi pia lilisema liliharibu mabomu ya kutegwa ardhini (IED), mikanda minne ya kujilipua na mahandaki 13 yaliyotumiwa na magaidi hao.

Vikosi vya Misri kwa miaka mingi vimepambana na uasi katika Rasi Sinai, ukiongozwa haswa na tawi la eneo la kundi la kigaidi la Daesh au ISIS.

Tangu Februari 2018, mamlaka imekuwa ikifanya operesheni ya kitaifa dhidi ya wanamgambo na magaidi, haswa ililenga Sinai Kaskazini na Jangwa la Magharibi la nchi hiyo.

Karibu wapiganaji 1060 wanaoshukiwa kuwa magaidi au wanamgambmo na makumi ya wafanyikazi wa usalama wameuawa huko Sinai, kulingana na takwimu rasmi.

Hakuna idadi ya waliokufa inayopatikana kwa njia huru kwani Sinai Kaskazini ni marufuku kwa waandishi wa habari.

3475397

Kishikizo: sinai misri daesh
captcha