IQNA

Sekta ya Halal kati ya mada kuu katika kikao cha Russia na Jukwaa la Kiuchumi wa Kiislamu

20:00 - July 31, 2021
Habari ID: 3474145
TEHRAN (IQNA) - Mkutano mkubwa wa kiuchumi kati ya Russia na nchi za Kiislamu maarufu kama Mkutano wa Kazan 2021 ulimalizika Ijumaa katika mji mkuu wa jamhuri ya Tatarstan katika Shirikisho la Russia

Hafla hiyo ya siku tatu ilivutia wageni 4,750 kutoka nchi 64.

Mikataba kadhaa ya ushirikiano katika nyanja anuwai kama vile kilimo, uundaji wa mashine, vyombo vya habari, na chakula ilifikiwa wakati wa mkutano huo.

Mkutano huo ulifanyika kwa kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Russia na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC). Washiriki katika kikao hicho walijadili masuala ya kifedha, sekta ya ‘Halal’, diplomasia ya vijana, dawa, michezo, tasnia ya ubunifu, uchukuzi na mawasiliano usafirishaji, biashara, na uwekezaji.

Maonyesho ya Halal ya Russia yalifanyika katika hafla hiyo, ambayo kaulimbiu yake kuu lilikuwa "matumizi yenye fahamu".

3475383

Kishikizo: russia halal
captcha