IQNA

Maelfu ya Wapalestina katika Sala ya Idul Adha + Video

18:34 - July 22, 2021
Habari ID: 3474117
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya waumini Wapalestina waslihisiri katika Sala ya Idul Adha iliyosaliwa katika Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) baada ya hujuma za siku kadhaa za Wazayuni dhidi ya Msikiti huo.

Wapalestina walikusanyika Jumane katika msikiti huo siku moja baada ya walowezi wa Kizayuni, wakipata himaya  ya wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel, waliuvamia msikiti huo.

Hayo yanajiri wakati ambao,Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na hujuma na uvamizi wake dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa na mji wa Quds.

Onyo hilo limo katika taarifa iliyotolewa na Ismail Hania, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiisloamu ya Palestina HAMAS ambaye amewaonya Wazayuni na kuwataka wasivuke mistari myekundu ya muqawama na Wapalestina.

Ismail Hania sambamba na kutoa mkono wa kheri na baraka kwa mnasaba wa kuadhimisha Sikukuu ya Eidul-Adh'ha amesisitiza kuwa, harakati ya muqawama imesimama kidete kutetea haki za taifa la Palestina na kwamba, katika vita vilivyopita vya Seif al-Quds muqawama ulimthibitishia adui nguvu ulionayo.

Aidha mkuu huuyo wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameeleza kuwa, njama na uvamizi wa hivi sasa wa Wazayuni ni kujitutumua na kutaka kufunika pigo walilopata na hivyo kufifiza ushindi mkubwa wa Wapalestina.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

3475306

captcha