IQNA

Sikiza adhana ya qarii maarufu wa Misri Ragheb Mustafa Ghalwash

TEHRAN (IQNA)- Hakuna shaka kuwa mmoja kati ya wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu nchini Misri alikuwa ni Ragheb Mustafa Ghalwash.

Mbali na sauti yake ya kipekee katika qiraa ya Qur'ani Tukufu, pia alikuwa na sauti yenye mvuto wakati wa kuadhini.

Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash  alizaliwa Julai 5 mwaka 1938 nchini Misri na kukulia katika familia iliyokuwa na mapenzi makubwa na Qur'ani. Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa tayari amehifadhi Qur'ani nzima katika rika la ubalobaro na kuanza kusoma kitabu hicho katika hafali na majlisi mbalimbali akiwa na umri wa miaka 16. Sheikh Raghib Mustafa Ghalwash alikuwa miongoni mwa wasomaji wa Qur'ani wa Misri walioalikwa mara kadhaa  katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sheikh Ghalwash aliaga dunia Februari 4 mwaka 2016 baada ya umri wa miaka 77 uliojaa baraka.

Hii hapa chini klipu ya Sheikh Ghalwash akiadhini.

3982346

Kishikizo: misri ، ghalwash ، adhana