IQNA

Sherehe ya kukumbuka kuzaliwa Imam Ridha AS yafanyika nchini Kenya

15:55 - June 22, 2021
Habari ID: 3474032
TEHRAN (IQNA)- Sherehe ya kukumbuka kuzaliwa Imam Ridha AS imefanyika nchini Kenya katika Kituo cha Kiislamu cha Jaafari mjini Nairobi kwa himaya ya Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Kenya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa Imam Ridha AS, Imam wa Nane wa Mashia,  kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Kenya  na Kituo cha Kiislamu cha Jaafari. Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa kidini (Husseiniya) katika Kituo cha Kiislamu cha Jaafari kwa kuzingatia kanunni za kiafya za kuzuia kuenea corona.

Miaka 1294 iliyopita, sawa na tarehe 11 Dhulqaada mwaka 148 Hijria, alizaliwa Imam Ali bin Mussa Ridha AS, mmoja kati ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW katika mji wa Madina.

Imam Ridha alichukua jukumu la kuwaongoza Waislamu mara baada ya kufariki dunia baba yake, Imam Mussa al-Kadhim AS, mnamo mwaka 183 Hijria. Shakhsia huyo alikuwa mbora zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu wakati wa zama zake. Kwa minajili hiyo, Ma'amun, Khalifa wa Kiabbasi alijaribu kumpatia wadhifa Imam Ridha AS kwa shabaha ya kuimarisha nafasi yake na wakati huo huo kumdhibiti mjukuu huyo wa Mtume. Imam Ridha AS alikubali pendekezo hilo kwa kulazimishwa na kwa mashinikizo ya utawala wa Ma'amun. Mtukufu huyo aliwaeleza Waislamu wote, wakiwemo watu wa eneo la Khorasan, ukweli wa mambo ulivyo, na kuwaathiri mno wananchi kuhusiana na uhakika wa Ahlul-Bait wa Mtume AS.

3979247

Kishikizo: imam ridha as kenya
captcha