IQNA

Sayyid Nasrallah ampongeza Sayyid Raeisi kwa ushindi uchaguzi Iran

18:02 - June 20, 2021
Habari ID: 3474023
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrallah amempongeza Sayyid Ebrahim Raeisi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uliofanyika Ijumaa.

Katika ujumbe wake, Nasrallah amesema Raesi ameleta matumaini katika taifa la Iran na mataifa mengine ya eneo kwa ushindi wake katika kipindi hiki muhimu katika historia ya Iran.

Amesema ushindi wa Raeisi pia unaleta matumaini kwa wanachi wa Irna na eneo zima kuhsu mustakabali na uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo.

 

Baada ya uchaguzi wa13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu uliofanyika Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran jana ilitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo ulioshirikisha mamilioni ya wapiga kura.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abdolreza Rahmani Fazli alitangaza matokeo hayo Jumamosi mbele ya waandishi wa habari hapa jijini Tehran na kusema kuwa, wapiga kura milioni 28 na laki tisa na 36 elfu na nne wameshiriki katika uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesema, asilimia 48.8  ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura wameshiriki kwenye uchaguzi huo. Ameongeza kuwa, Sayyid Ebrahem Raeisi ndiye aliyechaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kura milioni 17 na laki 9 na 25,345 za wananchi.

3978730/

captcha