Zoezi la kupiga kura lilimalizika Jumamosi (Juni 19) saa nane usiku, masaa 19 baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa saa moja asubuhi Ijumaa, Juni 18.
Muda wa zoezi la kupiga kura uliongezwa mara kadhaa ili kuhudumia idadi kubwa ya wapiga kura na pia kutokana na uzingatiaji wa kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Zaidi ya Wairani milioni 59 walikuwa wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ambao ulikuwa wa wagombea wanne baada ya Wagombea wengine watatu kujiondoa katika mchuano huo Jumatano.