Kwa mujibu wa taarifa Misahafu hiyo inaonyesha anua ya mitindo ya kaligrafia na sanaa zinginezo za Qur’ani kama vile Tadhib hasa zilizotumika wakati wa watawala wa zama za Uthmaniya.
Misahafu hiyo inamilikiwa na mwanakaligrafia maarufu wa UAE ambaye pia amezindua warsha ya kaligrafia katika maktaba hiyo.
Halikadhalika hutoa mafunzo ya namna ya kuandika aya za Qur’ani kwa mtindo ulio katika Misahafu ya kale. Amesema kuwa kuandaa maonyesho kama hayo kunawahimiza Waislamu kutunza Misahafu ya kale.