IQNA

Ustawi wa Mfumo wa Kiislamu wa benki nchini Afrika Kusini

20:13 - May 21, 2021
Habari ID: 3473933
TEHRAN (IQNA)- Kumeshuhudiwa ongezeko la utumizi wa huduma za Kiislamu za benki nchini Afrika Kusini kutokana na Waislamu kuzingatia zaidi mafundisho ya dini yao tukufu.

Kwa msingi huo,  Muungano wa Benki za Afrika Kusini (BASA) uliandaa kongamani la kwanza  mfumo wa kifedha wa Kiislamu mwezi Septemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa BASA, thamani ya huduma za kifedha za Kiislamu zilistawi na kufikia akiba ya Randi billion 35 mwaka 2019. Katika uga wa kimataifa thamani ya huduma za kifedha za Kiislamu ilikuwa na thamani ya dola trillion 2.

Naeem Ebrahim, mkuu Huduma za Kiislamu za Benki katika Benki ya FNB anasema huduma za Kiislamu katika benki zinatumiwa sana na Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu.

Mfumo wa Kiislamu wa fedha unaharamisha riba na hivyo unaendelea kuwavutia watu wengi duniani. Inakadiriwa kuwa mfumo wa Kiislamu wa kifedha sasa una ukubwa wa dola trilioni mbili kote duniani kuanzia Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), Afrika na Kusini mashariki mwa Asia.

3972782

captcha