IQNA

Safari ya Kihistoria ya Papa Francis nchini Iraq

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameitembelea Iraq katika safari ya kihistoria ambayo pia ni safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuibuka janga la COVID-19.
Papa Francis aliwasili Bagadad Ijumaa kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo akiwemo Rais Barham Salih.

Papa Francis pia amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Mashia wa Iraq Ayatullah Sayyid Ali al Sistani.