IQNA

Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran yaadhimisha miaka 40

20:24 - August 05, 2020
Habari ID: 3473037
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran (ACECR) amesema academia hiyo inapaswa kuongoza duniani katika ustawi wa sayansi na teknolojia.

Sayyid Hamid Ridha Tayyibi ameyasema hayo mjini Tehran Jumatano katika ofisi za IQNA wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 40 wa kuasisiwa  Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran.

Ameongeza kuwa, academia hiyo inapaswa kutoa mchango mkubwa katika kustawisha uchumi wenye msingi wa kiteknolojia na kuibua utamaduni mpya katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tayyibi amesema ACECR imeweza kupata mafanikio makubwa katika uga wa utamaduni na kuongeza kuwa, akademia hiyo ni taasisi ya kustawisha utamaduni.

 Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran, ambayo mmoja ya taasisi zake ni Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa (IQNA), ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 1980 kwa lengo la kustawisha utamaduni wa sayansi na teknolojia nchini Iran.

Mbali na kusimamia IQNA, harakati nyingine muhimu ya kimataifa ya ACECR ni kuandaa mashindano ya Qur’ani ya wanachuo Waislamu baada ya kila miaka miwili tokea mwaka 2006 kwa lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano baina ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu kote duniani sambamba na kustawisha kiwango cha harakati za Qur’ani katika vyuo vikuu.

 

3914855

captcha