IQNA

Palestina yalaani Israel kwa ujenzi wa vitongoji, yataka ICC ichukue hatua

19:05 - August 02, 2020
Habari ID: 3473024
TEHRAN (IQNA) -Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ichukue hatua za haraka za kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel hasa kitendo cha utawala huo kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imesema uchunguzi huo unapaswa kuanzishwa haraka ili maafisa watendai jinai wa Israel waweze kuadhibiwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Paletina imelaani kitendo cha wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuafiki ujenzi wa vitongoji viypa vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Mashariki la Al-Issawiya mashariki mwa mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu. Taarifa hiyo imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kusitishwa upanuzi wa viteongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imetahadharisha kuwa, uamuzi mpya wa utawala wa Kizayuni wa kuendelea na hatua zake za kivamizi dhidi ya Quds Tukufu na wakaazi wa mji huo unatekelezwa kwa lengo la kubadilisha ukwali wa mji huo pamoja na historia na utmabulisho wake.

Utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao unapata himaya kamili ya Marekani, umekiuka azimio 2334 la Baraza la Usalama, ambalo Disemba 2016 lilitaka usitishwaji wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. 

Karibu jamii nzima ya kimataifa inasisitiza kuwa hatua ya Israel kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi ni kinyume cha sheria.

3914176

 

captcha