TEHRAN (IQNA) – Waislamu wameanza kutekeleza ibada katika mji mtakatifu wa Makka.
Kufuatia kuibuka janga la COVID-19, idadi ya mahujaji mwaka huu ni 1,000 tu na wote ni wakaazi wa Saudi Arabia ambapo 700 miongoni mwao ni raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini humo. Hatua kali zimechukuliwa kuzuia kueneza ugonjwa wa COVID-19.