Moja kati ya qiraa zake mashuhuri ni hii iliyo hapa chini ambapo anaseoma aya za Sura An-Naziat ya 79 ya Qur’ani Tukufu kwa pumzi moja.
Katika klipu hii anasoma aya za 26 na 27 za Sura An-Naziat zisemazo: “Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!.”
Ustadh Mutawalii Abdul Aal alizaliwa Aprili 1947 katika familia yenye kuzingatia dini nchini Misri na aliweza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka 12. Baadaye alianza qiraa ya Qur’ani kwa kuiga mtindao ya usomaji wa Sheikh Abdulbasi na Sheikh Mustafa Ismail na hatimaye akaibua mtindo wake.
Alifanikiwa kutumbelea nchi mbali mbali duniani kama qarii na pia kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani.
Aliaga dunia Julai 16 akiwa na umri wa miaka 68.