IQNA

Msikiti mkubwa zaidi Afrika Magharibi wafunguliwa Senegal + Picha

17:09 - September 29, 2019
Habari ID: 3472153
TEHRAN (IQNA) – Makumi ya maelfu ya watu kutoka kote Senegal walijumuika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar, Ijumaa iliyopita kushuhudia kufungulwia rasmi msikiti ambao umetajwa kuwa mkubwa zaidi katika eneo la Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu walikuja kwa mabasi, magari binafsi na kwa miguu katika mtaa wa Bopp ulipo msikiti mpya unaojulikana na Masjid Masalik-al-Jinan, ambao una uwezo wa kubeba waumini 30,000.

Msikiti huo umejengwa na wafuasi wa harakati ya Tariqa ambayo inajulikana kama aṭ-Ṭariqat al-Muridiyyah ambayo inafuatwa na aghalabu ya Waislamu wa Senegal.

Ujenzi wa msikiti huo ulianza miaka 10 iliyopita katika ardhi yenye ukubwa wa ekari 14 ambayo ilitolewa na serikali ya nchi hiyo ambayo asilimia 90 ya raia wake ni Waislamu.

Jina la msikiti huo, Masalik-al-Jinan (Njia za Kuelekea Peponi), limetokana na anwani ya shairi ambalo lilitungwa Sheikh Ahmadou Bamba Mbacke, ambaye aliasisi Tariqa hiyo karne ya 19 Miladia.

Msikiti huo ambao kuta zake za nje zimepambwa kwa marumaru aina ya Carrara na minara mitano, mrefu zaidi ukiwa wa mita 78 una uwezo wa kubeba waumini 15,000 ndani na wengine 15,000 kwa uwanje wa nje ya msikiti. Inatazamiwa kuwa katika siku za usoni kandoni mwa msikiti huo kutajengwa kituo cha Kiislamu, nyumba za makazi na jumba la makumbusho.

Ujenzi wa msikiti huo umegharimu Euro millioni 30 kutoka kwa wafadhili binafsi huku mchango wa serikali ukiwa ni takribani Euro milioni 10.5.

Kiongozi wa aṭ-Ṭariqat al-Muridiyyah, Mountakha Mbacke, amepokea idadi kubwa ya wageni wa kidini, kijadi na kisiasa wakati wa uzinduzi wa msikiti huo. Aidha msikiti huo una quba lenye rangi ya dhahabu na ndani kuna taa kubwa aina ya chandelier pamoja na nakshi zilizochorwa na wataalamu kutoka Morocco.

Sherehe za ufunguzi wa Masjid Masalik-al-Jinan zimehudhuriwa na Rais Macky Sall wa Senegal na rais wa zamani wa nchi hiyo Abdoulaye Wade, ambao wamepata taufiki ya kupeana mkono baada ya muda mrefu wa uhusiano uliojaa uhasama.

Aṭ-Ṭariqat al-Muridiyyah ni kati ya makundi manne muhimu ya Tariqa ambayo hufuatwa na Waislamu wa Senegal.

3845378

captcha