IQNA

Kwa ushiriki wa Iran

Kikao cha Mabunge ya Nchi za Kiislamu chafanyika Iraq

0:09 - January 26, 2016
Habari ID: 3470089
Kikao cha 11 cha Umoja wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kimefanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Katika awamu ya kwanza, kikao hicho  kilifanyika katika ngazi ya wabunge na kisha kufuatiwa na kikao cha maspika wa mabunge hayo kilichofanyika kwa muda wa siku mbili kuanza Jumapili na kuendelea hadi Jumatatu.
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameiwakilisha Iran katiak kikao hicho ambapo amesisitiza umuhimu mkutano huo Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
Kongamano hilo limefanika kwa lengo la kutafuta stratijia ya pamoja katika kukabiliana na misimamo mikali na ugaidi duniani.
Mbali na Iran nchi zingine ambazo zimeshiriki katika kikao hicho ni kama vile Uturuki, Pakistan, Mali, Algeria, Kuwait, Syria, Sudan, Tunisia na Somalia.
Wakati huo huo

Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kutuma misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina waliozingirwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Akizungumza  Jumatatu wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Iraq Salim al-Jabouri mjini Baghdad pambizoni mwa mkutano wa 11 wa Umoja wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PIUC), Larijani amebainisha kusikitishwa kwake kwa kuona kuwa, Waislamu hadi sasa wameshindwa kutekeleza majukumu yao kuhusu Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, eneo ambalo limekuwa chini ya mzingiro wa Israel kwa takribani miaka 10 sasa.

Katika mazungumzo hayo Spika wa Bunge la Iran pia amebainisha kuridhishwa kwake na hali ya usalama ilivyo hivi sasa nchini Iraq kufuatia hatua zilizochukuliwa katika kukabiliana na kundi la kigaidi la Daesh au ISIS .

Larijani aidha amesisitiza kuhusu umoja na mshikamano kati ya makundi mbalimbali ya Wairaqi. Kwa upande wake Spika wa Bunge la Iraq ameelezea matumaini yake kuwa, nchi za eneo hili zitaweza kupata utatuzi wa hitilafu zilizopo baina yao.


3469964
captcha